Ad Code

Maamuzi Ya Kikao Cha Kamati Ya Uendeshaji Na Usimamizi Wa ligi Ya Bodi Ya Ligi Kuu Cha February 10, 2022

NBC Tanzania Premier League, Tanzania Premier League Board, Bodi ya Ligi kuu Tanzania, Kikao cha uendeshaji na usimamizi wa ligi, Adhabu za waamuzi (referees) walochezesha mechi za Simba na Yanga ligi 2021/2022, mechi za ligi kuu, Adhabu ya mchezaji wa Yanga Dickson Job, Adhabu ya wasemaji wa Yanga Haji Manara na Hassan Bumbuli, Ligi Kuu ya Tanzania Bara.


Maamuzi ya kikao cha kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi kuu tanzania bara kilichofanyika tarehe 10 january 2022



KAMATI ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha february 10, 2022 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi yafuatayo:-

Ligi Kuu ya NBC (NBCPL)

➤Mechi Namba 105: kati ya KMC FC 1-1 Biashara United FC

Klabu za KMC FC na Biashara United zimepigwa faini ya Tsh 1,000,000 (milioni moja) kila mmoja kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina

Katika mchezo tajwa hapo juu kwenye uwanja wa Azam Complex, KMC na Biashara vilishindwa kutoka vyumbani kwa wakati ulopangwa kwenye ratiba ya matukio ya mchezo, kwa kile kilichoonekana kila timu iwe ya mwisho kutoka.

Wachezaji wa timu hizo walionekana kuchungulia nje ili kujirizisha kama timu pinzani imeshatoka, tukio lililosababisha mchezo kuchelewa kwa muda wa dakika mbili (2)

kitendo cha mchezo kuchelewa kuanza kimekua na athari kubwa kwa mdhamini wa ligi kuu ya NBC mwenye haki za matangazo ya runinga (Azam Media Limited) kwani kulivuruga ratiba za matangazo yao.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni ya 47(30) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

➤Mechi namba 109: kati ya Young Africans SC 0-0 Mbeya City FC

Mwamuzi wa kati, Hussein Athumani kutoka Katavi na mwamuzi msaidizi namba mbili, Godfrey Msakila wa mkoani Geita wameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko (3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu katika mchezo tajwa hapo juu ulochezwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa February 5, 2022.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni ya 42:1(1.1) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi.

Pia klabu ya Yanga (Young African) imetozwa faini ya Tsh 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabki zake kuwarushia chupa za maji waamuzi wakati wakielekea katika vyumba vya kuvalia mara baada ya mchezo taja hapo juu kumalizika.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni ya 47(1) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

Klabu ya yanga imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuwakilisha maafisa wanne(4) tu badala ya watano(5) kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo tajwa hapo juu

Onyo hili ni kwa uzingativu wa kanuni ya 17:2(2.1.1) ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Pia Mchezaji wa klabu ya Yanga, Dickson Job amefungiwa michezo mitatu(3) na kutozwa faini ya Tsh 500,000(laki tano) kwa kosa la kumkanyaga kwenye mbavu mchezaji wa Mbeya city, Richard Ng'ondya jambo lililotafsiriwa kua ni mchezo wa hatari.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni ya 41:5(5.3) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

➤Mechi Namba 112: Simba 1-0 Tanzania Prisons FC

Mwamuzi wa kati, Ahmada Simba kutoka Kagera ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko (3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mchezo wa mpira wa miguu katika mchezo tajwa hapo juu ulochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa February 3, 2022.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni ya 42:1(1.1) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi.

Matukio kwenye mikutano ya wanahabari

Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya yanga, Hassan Bumbuli na Haji Manara wametozwa faini ya Tsh 500,000(laki tano) kila mmoja kwa kosa la kuwashutumu waamuzi wa ligi kuu ya NBC kupitia vyombo vya habari.

Bumbuli na Haji walizungumza na Waandishi wa habari February 8, 2022 kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu ya yanga ambapo walishitumu waamuzi wa ligi kuu kwa masuala mbalimbali waliyoyahusisha na upendeleo, wakitaja matkio kadhaa yakiwemo ya kuongeza dakika zaidi kwenye muda wa nyongeza katka michezo ya klabu ya simba.

Kwa mujibu wa sheria namba tano (5) ya mpira wa miguu, mtunza muda katika mechi ni waamuzi pekee, hivyo kamati imetoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kuhoji suala la muda wa nyongeza katika mechi za ligi.



Ad Code