Ally Sonso, Ruvu Shooting FC, Yanga, Kagera Sugar FC, Lipuli FC, Young African, NBC Premier League, Tanzania Premier League Board, Beki wa Zamani wa Yanga Ally Sonso
Beki wa zamani wa Yanga ambaye alikuwa anaichezea Ruvu Shooting Ally Mtoni Sonso amefariki Dunia tarehe 11/02/2022 muda mchache wakati akipelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuuguza mguu wake tangu mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Simba Sc ulochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Sonso ambae alikua akiichezea Ruvu shooting mpaka umauti ulipomkuta, imeelezwa alikua akiuguza majeraha ya mguu tangu October mwaka jana 2021 Ally Sonso enzi za uhai wake amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali vikiwemo Yanga, Kagera Sugar, Lipuli na Ruvu Shooting
Ally Abdukarim Ibrahim Mtoni, akijulikana zaidi kwa jina la Ally Sonso alizaliwa March 13, 1993 amefariki February 11, 2022 akiwa na umri wa miaka 29. Ally Sonso alikua ni mchezaji wa mpira wa migu Mtanzania aliekua akicheza nafasi ya Beki (Defender).
Mbali na kuchezea timu za Kagera Sugar, Lipuli fc, Young Africans sc, lakini pia Ally sonso amewahi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania mwaka 2018 na mwaka 2019
Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Social Plugin