Kenya, Tanzania, Mombasa, Dar es salaam
Habari kubwa kutoka nchini kenya wikiendi hii ambayo imeandikwa na magazeti maarufu zaidi kutoka nchini humo kupitia tovuti zake
Gazeti la Standardmedia.co.ke, wameandika kichwa cha habari kinachosema:-
Alikiba's wife files for divorce, demands Ksh 200,000 monthly upkeep
Gazeti lingine kupitia tovuti yake ya The STAR, nao wameandika kichwa cha habari kinachosema:-
Alikibika given 15 days to respond to Divorce sult
Taarifa zinasema;
Alikiba amepewa siku 15 kujibu kesi ya talaka iliyofunguliwa na mkewe mkenya, Amina Khalifu aliyefunga nae ndoa mwezi April 19, 2018 na sasa wakiwa na watoto wawili(2)
Alikiba analalamikwa kutelekeza ndoa yake
Bi. Amina ameeleza sababu mbalimbali kama Usaliti kwenye ndoa, Kutukanwa pamoja na Kero kutoka kwa ndugu wa mumewe ni miongoni mwa sababu zilizofanya atake kujiondoa kwenye ndoa hiyo
Amina amesema hayo yalianza miezi sita(6) tu baada ya ndoa yao
February 10, 2022 Mahakama ya Kadhi ya Mjini Mombasa ilimpa alikiba siku 15 ambapo kama hasipofanya kutii wito huo, mchakato wa talaka utaendelea bila ya uwepo wake
Agizo la Mahakama ya Kadhi lilisomeka;
Kama utashindwa kutokea kwenye muda uliotajwa hapo juu, mlalamikaji ataendelea na kesi na hukumu itatolewa bila ya uwepo wako mahakamani
Kwa mujibu wa Nyaraka za mahakama ambazo gazeti la The STAR limesema wameziona, January 8, 2021 Amina alihamia Mahakama ya Kadhi akitaka kuondoka kwenye ndoa hiyo na Alikiba
Kwenye mashitaka yake, Amina alidai kuwa hakua akipewa mazingira salama na mshikamano alipokua ukweni jijini Dar es salaam
Mlalamikiwa Alikiba amekua akipuuza ndoa yake ambapo pasipo heshima alionyesha vitendo vya usaliti na wanawake mbalimbali bila kujali hisia za mlalamikaji, Nyaraka za mashtaka yake zimesema.
Amina anasema baada ya kuzaliwa mtoto wa kwanza February 19,2019 Alikiba alikua akimuacha bila chakula au mahitaji ya msingi wakati wakiishi wote ukweni jijini Dar es salaam na wakati huo alikua akinyonyesha
Amina amesema licha ya kutafuta suluhu ya matatizo yao, Alikiba hakua tayari na hakuonyesha kujari jitihada hizo za mkewe
Iko wazi kuwa mlalamikiwa Alikiba amekua akitenda katika mwenendo ambao hautarajiwi kwa mtu alieoa na ishara ya kutojari kabisa hisia za mlalamikaji na hivyo kusababisha maumivu, mateso, kuteseka kiakili (depression) na kuteseka kisaiklojia. zinasomeka nyaraka hizo za mahakama
Amina alisema "ndoa hii imevunjika vibaya na hakuna nafasi ya kuiokoa tena"
Amina anataka ndoa hiyo ivunjike na anataka kupewa Sh 200, 000 za Kenya ambazo ni zaidi ya 4,000,000 (million nne) za Tanzania kila mwezi kwa ajili yake na malezi ya watoto wao.
Alikiba pia anapaswa kugharamikia matibabu ya wanae wanapougua
Hii ni taarifa mpya kupitia media za Kenya kama The Standard na The STAR
Read aslo: Diamond Platnumz EP #FOA
Social Plugin