Ad Code

USGN Vs Simba SC today

Simba Sc ya Tanzania, Dar es salaam dhidi ya USGN ya Niger leo Tarehe 20/2/2022

 

Starting Simba players Vs USGN

Wawakilishi wa mashindano ya CAF Confederation Cup, Simba SC ya Dar es salaam, leo inaikabiri timu ya Union Sportive Gendarmerie Nationale (USGN) ya Niger kwenye kundi lao group D ikiwa ni mchezo wao wa pili kwenye uwanja wa Général Seyni Kountche in Niamey, Niger. Simba wako ugenini katika mchezo huo

Union Sportive Gendarmerie Nationale FC of Niger

Mchezo huu unachezwa 7pm leo Jumapili 20/2/2022 majira ya Tanzania.

Simba wanahitaji ushindi katika mchezo huu kwa ajili ya kujitengenezea nafasi nzuri ya kuingia katika hatua na mtoano

Pia, Leo RS Berkane ya nchini Morocco inacheza ugenini (away) dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast kwenye match nyingine ya kundi D inayochezwa katika uwanja wa de l’Amitié Général Mathieu Kérékou in Benin.

Kwenye match yao ya kwanza, Simba sc walishinda 3-1 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium Dar es Salaam.

USGN wao walipoteza 5-3 dhidi ya RS Berkane wakiwa ugenini.

Kocha mkuu wa Simba sc, Pablo Franco alisema wanaikabiri timu ngumu lakini wanategemea ushindi

"Inaenda kua game ngumu ikiwa USGN ni moja kati ya timu ngumu kwenye mashindano haya," Alisema Pablo

Kocha Pablo amesema wako tayari kwa mpambano japokua baadhi ya wachezaji wao muhimu hawatacheza match hiyo.

Wachezaji hao ni Larry Bwalya na Mzamiru Yasin, wanaokabiriwa na matatizo ya kifamilia. Pia Hassan Dilunga, Kibu Deniss na Chriss Mugalu wao ni majeruhi na wanaendelea na matibabu.

Simba Vs USGN Result/Matokeo Ya leo

USGN Vs Simba sc Results






Simba imefanikiwa kutoka sare ya 1-1 na USGN ikiwa ugenini matokeo ambayo yanamfanya Simba kuliongoza kundi lao Group D wakiwa na Point 4 wakifuatiwa na RS Berkane

Bao la Simba limefungwa na mchezaji wao Bernard Morrison dakika ya 84 Assist ikitoka kwa Kapombe.

Bernard Morrison aliingia dakika ya 65 kama substitution akichukua nafasi ya midfielder Yusufu Valentine Mhilu

RS Berkane wao wamepoteza mchezo wao dhidi ya Asec Mimosas ambao walikua nyumbani kwa magoli 3-1

Asec Mimosas Vs RS Berkane Results

Group D CAF Confederation Cup Standings

Group D CAF Confederation Standings


Ad Code